Kanisa la Kipentekoste lenye msingi na imani katika Neno la Mungu linaloundwa na ujumla wa makanisa mahalia pamoja. Lilianzishwa chini ya wamisionari kutoka Kanada wakiwa chini ya Shirika la kimisionari liitwalo Pentecostal Assemblies of Canada ambao walianza kueneza Injili Tanganyika katika miaka ya 1912 ambapo katika miaka hiyo wengine walifariki kwa magonjwa.
Mnamo mwaka 1950, wahubiri wa mwanzo wa Tanganyika walipewa mafunzo. Kanisa lilianza katika mkoa wa Mara na kuanzisha shule ya Biblia pale Nyasirori Butiama. Wakati huo lengo kuu lilikuwa kuhubiri Injili na kuanzisha makanisa. Kanisa liandikishwe rasmi mnamo tarehe 14 Aprili mwaka 1967 na kupata "Cheti cha Ithibati"
Historia kamili inaonesha kuwa wamishenari wa kwanza kabisa kutoka Kanada waliingia Tanganyika miaka ya 1913, na kuanzisha kazi ya Mungu maeneo ya Itigi, mkoani Singida, lakini kazi hiyo haikusimama. Katika mwaka 1940 baadhi ya wakristo kutoka Kenya ndugu Elly Osumba na wenzake wanne wakahamia Tanganyika mkoa wa Mara huko Bugwema, Nyangombe Majita, wakaanza ibada ya jumapili chini ya mti. Mwaka 1944 Mwinjilisti kutoka Kenya Athanasio Odenyo Okech akaja kusaidia kazi hiyo. Jengo la kanisa la kwanza la miti lilijengwa mwaka 1946 na wakati huohuo kanisa la Pentecostal Assemblies of God Kenya wamisionari wawili Rev. Morrison na Rev. J. Liny na wachungaji wawili Rev. Charles Muga na Rev. James Gorgor wakafanya ubatizo wa kwanza Tanganyika. Walibatiza watu kumi, kanisa wakati huo linaitwa Pentecostal Assemblies of God East Afrika (PAGEA).
Juhudi na taabu walizopata watumishi wenzetu waliopita wakimtegemea Mungu, matunda yake ndiyo haya yanayoonekana hivi leo. PAG (Tanzania) tulijitegemea wenyewe mwaka 1967 na kupata cheti cha ithibati “Certificate of Incorparation” tarehe 14/04/1967. Uchaguzi mkuu wa kwanza ulifanyika oktoba 1967 na akachaguliwa Askofu mkuu wa kwanza Rev. Jacson Magarinza. Uchaguzi mkuu wa pili mwaka 1969 – Askofu mkuu Rev.Herman Ndenda. Uchaguzi mkuu wa tatu na nne 1971-1975 – Askofu mkuu Rev. Jacson Magarinza. Uchaguzi wa mkuu wa tano na sita 1975-1978 – Askofu mkuu Rev. Stephen Omoso. Uchaguzi mkuu wa saba, nane, tisa, na kumi 1979-1985 – Askofu mkuu Rev. Daniel Itaja. Uchaguzi mkuu wa kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu mwaka 1993-2005 Askofu Rev. Francis Rwechungura. Uchaguzi wa kumi na nne mwaka 2005-2010 Kanisa likiwa pande mbili upande moja alichaguliwa Askofu Rev. Daniel Awet. Na upande mwengine akachaguliwa Askofu Thomas Faida. Mwaka wa 2013 ukafanyika uchaguzi wa kumi na tano wa pamoja akachaguliwa Askofu Dr. Daniel Awet.
ASKOFU MKUU PAG (T)
"Yeremia 33:3" "Niite, nami nitakuitikia na kukuonyesha mambo makubwa yaliyo fichika ambayo hujapata kuyajua"
VIONGOZI WA IDARA MBALIMBALI
Tunakupongeza Askofu Mkuu Mteule wa TAG Rev. Dr. Barnabas Mtokambali na Kamati Yako kwa kuchaguliwa. Soma zaidi
Mwaka huu 2024 tarehe 25 - 27 September kutafanyika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi. Soma zaidi
Askofu Mkuu na Mhasibu Mkuu wakizawadiwa na Kanisa Soma zaidi
Ev. Philip S. Amos katika majukumu ya uinjilisti katika viwanja vya makulu... Soma zaidi
Tukio hili limefanyika katika kanisa la Luhembe na Mruklazo (Jimbo la Kagera wilaya ya Ngara), ambapo msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kama daftari na vinginevyo Soma zaidi
Ni makabidhiano ya gari. Soma zaidi